adventure254

« »

Tuesday, February 7, 2012

UMUHIMU WA UTALII NCHINI

After all I just discovered my written Swahili isn’t that bad like the one I speak (characterized by –di and –ndis, -chi and –shis bombarding each other unceremoniously).I chose a simple topic to start with and the following is the importance of tourism to Kenya according to me in Swahili.
  Utalii ni hali ya kusafiri huku na huko kuyafurahia mandhari. Pia kule kushughulikia watalii au kuwahudumia ni Utalii. Hapa nchini, utalii huchukuliwa kama kitendo cha kusafiri mbali na mahali unakoishi, mfano kutoka Kenya kwenda Uganda ama pia kutoka Nairobi kwenda kujivijari Nakuru. Kwa ufupi kuna viwango viwili vya utalii; kuna kule kutembea kutoka mahali pamoja hadi pengine katika nchi yako, almaarufu kama Domestic Tourism kwa lugha ya kimombo na kuna kutoka nchi moja hadi nyengine.
Hapa Kenya Utalii umedhaminiwa sana kwani huchangia pakubwa kuinua uchumi wa nchi. Mwanzo, vinavyovutia watalii hapa nchini ni wanyama wa porini, pwani ya Kenya, vitu vya kihistoria, mila na utamaduni na hata mazingira.
Watalii wanaotoka nchi za kigeni huleta fedha za kigeni na hivyo kuimarisha uchumi wa nchi kwani hutumiwa kununulia vitu vingine na kukuza maendeleo nchini. Utalii pia unasaidia kuimarisha idadi ya nafasi za kazi za adinasi farafara nchini. Watu wanavyozidi kupata kazi ndivyo uchumi unazidi kuimarika na umasikini kupungua.
Kupitia utalii, kuna utunzaji wa mazingira. Mjinga pekee ndiye atakayekwambia mvua hutoka ‘mbinguni’. Miti huleta mvua. Kwa hivyo utunzaji wa mazingira unasaidia pakubwa kuongeza idadi ya mvua katika sehemu mbalambali nchini. Zaidi ya hayo, miti huwa chakula na mahali pakuishi pa wanyama wengi.
Watalii wawekezaji ambao wengi wao huwa wakwasi wenye mbango si haba, huwekeza katika sekta mbalimbali nchini. Wao hulipa ushuru mwingi na hivyo basi kuimarisha uchumi wa nchi.
Watalii wengi huchukua ‘picha’ za wanakotembelea na wanayoona na kisha kuwaonyesha wenzao wanaporudi nyumbani. Hii huwapa wengine hamu ya kutembea Afrika na hapa nchini na hivyo kuongeza idadi ya watalii nchini. Idadi ya watalii inavyoongezeka, ndivyo mapato kutokana na utalii yanavyozidi kuongezeka.
Hata wewe unapozuru sehemu mbalimbali hapa nchini, unajiwezesha kufahamu nchi yako vizuri. Tembelea #TEMBEA KENYA  kwenye tovuti ya Magical Kenya ujionee mengi.
To translate from Swahili to English click here

No comments:

Post a Comment

About the Author

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...